Home/Journal of Kiswahili and Other African Languages/Article Record
Peer-Reviewed Article March 16, 2026

Uasi au Utatu katika Ujitambulishaji wa Wanajenizi: Matumizi ya Mihadarati katika Nyimbo za Gengetone

Are you an author of this work?Link to your sovereign AfriScholar profile
Published in: Journal of Kiswahili and Other African Languages
Publisher: Not stated • Kenya • 2958-4914
DOI: https://doi.org/10.58721/jkal.v4i1.1551

Abstract

Makala hii inahusu matumizi ya uasi ndani ya utatu kama mkakati wa kutambulisha vijana wa Jenizi kupitia nyimbo za Gengetone. Fasihi simulizi kupitia kipera kimojawapo cha nyimbo za gengetone, inatumiwa kupinga na au kuhimiza matumizi ya mihadarati kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali. Kwa jicho la haraka, inaonekana kuwa, baadhi ya waimbaji wa gengetone wanashabikiwa ukiukaji wa ukawaida wa kijami. Hata hvivo, kwa kutumia jicho la ndani, imebainika kuwa, wasanii hawa wanapinga mifumo dhalimu ya kijamii na kupendekeza mwamko mpya. Kwa hivyo, ni muhimu kuchanganua nyimbo teule za gengetone kwa jicho la ndani ili kubainisha kiini chake. Kutokana na haya, makala hii inachunguza mikakati inayotumiwa kuasi ukawaida, matumizi ya uasi kama silka ya ujitambulishaji; na matumizi ya utatu kama mkakati wa kupinga unyanyaswaji wa wanyonge kupitia nyimbo za gengetone. Haya yamebainishwa katika makala haya, ambapo uchambuzi wa nyimbo tano za gengetone umefanywa kwa kuongozwa na Nadharia ya Utatu. Uchambuzi wa data katika makala hii umedhihirisha kwamba nyimbo za Gengetone zinakua kwa kasi kikubwa sana kutokana na uwezo wake wa kujinyambua, ili kupanua mipaka yake. Ujinyambuaji huu unafanywa kwa kuchopeka mitindo mipya ili kuendelea kuwa hai, kuvutia na kusisimua. Isitoshe, Gengetone siyo tu aina ya muziki, bali ni aina maalum ya ujitambulishaji wa vijana wa mjini. Huu ni mfano mzuri wa nguvu za sanaa zinazotumiwa kuvunja kuta za ukabila, kuunganisha tamaduni mbalimbali, na kutoa jukwaa la kuwawezesha vijana kutoa sauti zao. Ni jukwaa la utatu ambalo linaloonesha ukakamavu, ubunifu na uzalendo wa vijana wa mjini.

Download Full Text PDFCrossref RecordCrossref XML

Verified Citation Velocity

Recorded scholarly citations in African and international peer-reviewed literature

0
Total Citations

Citations are continuously tracked and harvested across continental OJS endpoints and OpenAlex feeds.